Mradi wa kuhifadhi Chakula katika kanda ya Songea unajenga vihenge vya kisasa (silos) 12 vyenye uwezo wa kuhifadhi nafaka tani 45,000 na maghala mawili yenye jumla ya tani 10,000 kwa fedha za serikali shilingi bilioni 23.37.
Kukamilika kwa mradi huu kutaifanya Kanda ya Songea kuwa na uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 84,000 ndani ya maghala na vihenge kwa wakati mmoja.
Pamoja na vihenge hivi vya kisasa, mradi pia unajenga miundombinu wezeshi kama stoo ya vifaa, stoo ya viuatitifu, ujenzi wa ofisi, ujenzi wa maabara, ujenzi wa vyoo, kantini, uzio na barabara za ndani.
Hata hivyo mradi wa kuhifadhi chakula Kanda ya Songea hivi sasa una Maghala sita yenye uwezo wa kuhifadhi tani 29,000 za nafaka.
Mradi katika kanda ya Songea unajengwa na mkandarasi kutoka nchini Poland kwa kushirikiana na kampuni ya kitanzania ya Civil Loth.
Hadi sasa utekelezaji wa mradi umefika zaidi ya asilimia 71.75 ambapo ujenzi na usimikaji wa vihenge umefikia wastani wa asilimia 86, ujenzi wa maghala na miundombinu mingine umefikia asilimia 38.
Imeandikwa na Albano Midelo,Afisa Habari wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.