I
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, anatarajia kuzindua rasmi maonesho ya NaneNane tarehe 01.08.2023 ambapo Kitaifa yatafanyikia Jijini Mbeya katika Viwanja vya Nanenane vya John Mwakangale, kama zilivyo fursa nyingine hii pia ni moja ya fursa adhimu kwa wakulima na wafugaji kujifunza namna ya kufuga na kulima kisasa, kwa kutumia fursa mbali mbali zinazotolewa na Serikali, ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA WA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA”
Kama ilivyo kwa Halmashauri nyingine katika mikoa ya Tanzania, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, nayo ni miongoni mwa Halmashauri ambazo zitatoa huduma kwa wakulima, wafugaji na wananchi wengine, kwa siku kumi mfululizo kwanzia tarehe 1/08/2023 mpaka tarehe 10/08/2023, ambapo kwa upande wa Nyanda za juu kusini, itafanyika Jijini Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndg. Neema M. Maghembe, anawakaribisha wananchi wote kwenye maonesho hayo, kwa ajili ya kupata Elimu kuhusu mambo mbalimbali yanayotolewa na wataalamu wetu, ambao kupitia fursa hiyo wanaweza kujiajiri na kuongeza kipato kwao, familia zao na Taifa kwa ujumla.
Pamoja na hayo, mtaalam mwenye dhamana ya kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Songea Ndg. Hellen Shemzigwa, pia ametoa wito kwa wakulima, wafugaji na wajasiriamali, kwenda kujifunza namna na njia rahisi ya kulima mazao ya kibiashara, na namna ya kufuga mifugo tofauti, tofauti kwa kutumia mbinu rahisi na za kisasa.
Miongoni mwa mifugo ambayo, Halmashauri ya Wilaya ya Songea itatoa elimu, ni pamoja na ufugaji wa Samaki, ufugaji wa ng’ombe wa kisasa, ufugaji wa kuku, bata na ufugaji wa nyuki.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.