Halmashauri ya Manispaa ya Songea imetumia shilingi milioni 30 kwa ajili ya utengenezaji madawati 500,yatakayotumika kwa wanafunzi wa shule ya Msingi na Sekondari.
Kwa mujibu Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Songea Zakia Fandey Idara inatarajia kugawa madawati 200 yenye thamani ya sh.milioni 10, ikiwa ni fedha za mapato ya ndani ya bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020.
“Mahitaji ya madawati kwa sasa katika shule za msingi Manispaa ya Songea ni 17822, madawati yaliyopo ni 14958 na pungufu ni 2864’’,alisema.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Manispaa ya Songea katika Bajeti 2020/2021,imetenga zaidi ya shilingi milioni 20 ambayo itatumika kutengeneza madawati 400.
Naye Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Songea Devota Luwungo, amesema Idara yake inatarajia kugawa Viti na Meza 300 vyenye thamani ya sh.milioni 20 ikiwa ni fedha za mapato ya ndani Bajeti ya 2019/2020.
Hata hivyo amesema, Mahitaji ya meza kwa sasa ni 15214, yaliyopo kwa sasa ni 9733, upungufu ni 5481 ambapo mahitaji halisi ya viti kwa sasa ni 15214, yaliyopo ni 9990, na pungufu ni 5224.
Aidha katika kutatua changamoto katika shule za sekondari, Manispaa ya Songea katika mwaka 2020/2021,imetenga zaidi ya sh.milioni 15 kwa ajili ya kutengeneza viti na meza 230.
Manispaa ya Songea ina shule za msingi 94 na shule za sekondari 40.
Imeandaliwa na Amina Pilly
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Februari 6,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.