Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kupitia Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imeendesha zoezi la kuhamasisha unywaji wa maziwa ili kuwajengea wananchi tabia ya kunywa maziwa yenye viini lishe vya kutosha vya kuupa mwili mahitaji mhimu ili kukabiliana na utapiamlo na udumavu.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika katika shule za msingi Mahenge na Litembo, Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Haruna Masige amebainisha kuwa maziwa yana viini lishe vya kutosha kama vile protini,vitamini, mafuta, wanga pamoja na madini ya calcium na phosphorus ambavyo ni mhimu sana katika ukuaji na kuboreshaji wa afya.
Wilaya ya Mbinga inaendesha zoezi hilo ili kuunga mkoni jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt,Samia Suluhu Hassan za kuimarisha lishe na kutokomeza utapiamlo na udumavu nchini
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.