HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imefikia lengo la utoaji dawa za Kinga tiba za Usubi kwa kuwafikia wananchi 229, 414 sawa na asilimia 100. 4 ukilinganisha na mwaka 2022 ambapo zoezi hili lilifanikiwa kwa asilimia 84.
Kwa mwaka 2023 zoezi la utoaji dawa za Kinga tiba katika ngazi ya jamii lililenga kuwafikia wananchi 228,466 waishio katika viunga vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Kaimu Mkuu wa Idara ya huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Dkt. Amad Mwalukungu ameeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na muitikio mkubwa wa wananchi baada ya kupatiwa elimu juu ya faida ya dawa za Kinga tiba za Usubi.
" Tumefikia lengo tulilojiwekea , na kabla ya yote tulitoa elimu ya kutosha na hii imesaidia sana wananchi kujitokeza na kumeza dawa" Amebainisha Mwalukunga
Amefafanua kuwa zoezi hili la utoaji wa dawa za Kinga tiba za Usubi lilitekelezwa kwa siku saba kuanzia tarehe 17 hadi 23 mwezi Agosti katika Kata 29 za Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Kwa upande wake Mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Joseph Washa Washa amebainisha kuwa zoezi hili liliratibiwa kwa kuwafuata wananchi katika Kaya zao ( nyumba kwa nyumba), hatua hii imewapunguzia gharama wananchi na kuwaondolea usumbufu wa kwenda katika vituo vya afya kupata huduma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.