Mbunge wa Jimbo la Madaba, Wilayani Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Joseph Kizito Mhagama, ameongoza uzinduzi wa ujenzi wa stendi mpya katika Kijiji cha Lituta, Kitongoji cha Kifagulo.
Stendi hiyo mpya inatarajiwa kuboresha huduma za usafiri na uchumi wa eneo hilo.
Katika hotuba yake, Mhagama alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha za mradi huo.
Alieleza kuwa ujenzi wa stendi hiyo utagharimu takriban shilingi bilioni tano hadi kukamilika.
Pia alibainisha kuwa mradi huu ni miongoni mwa miradi mikubwa inayoendelea ndani ya Halmashauri ya Madaba, ikiwemo mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 5.5 katika Kata ya Mtyangimbole.
Mhandisi wa Halmashauri ya Madaba, Jeremiah Chambai, aliwasilisha ramani ya mradi huo na kueleza jinsi standi hiyo itakavyokuwa baada ya kukamilika.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba, Abdul Manga, alithibitisha kuwa tayari shilingi milioni 205 zimepokelewa kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Aliongeza kuwa ujenzi utaanza wiki ijayo kama ilivyopangwa, huku akiwataka wananchi kushirikiana kikamilifu kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.