Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge Wawakilishi wa Umoja wa Mabunge Duniani kutoka Tanzania, ameongoza msafara wa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushiriki Mkutano wa 150 wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea mjini Kashkenti, Uzbekistan kuanzia Aprili 5 hadi 9, 2025.
Katika mkutano huo, Mhagama aliwasilisha juhudi za Bunge la Tanzania katika kuisimamia serikali na kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kikamilifu, hasa katika nyanja za maendeleo na haki za binadamu. Alieleza namna Bunge linavyohakikisha uwajibikaji na usawa kwa jamii.
Mkutano huo unazungumzia nafasi ya Mabunge katika kupigania maendeleo na haki za jamii (Social Development and Justice). Tanzania imetambuliwa kwa nafasi yake muhimu katika kuhamasisha na kutunga sheria zenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi wake.
Mhagama alifafanua hatua mbalimbali ambazo Tanzania imechukua katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kulinda haki za binadamu. Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Mabunge duniani katika kufanikisha malengo ya pamoja ya maendeleo endelevu.
Mkutano huu umetajwa kuwa wa kihistoria na umeipa Tanzania fursa ya kuonyesha mchango wake katika masuala ya msingi ya haki na maendeleo, huku ikiendelea kujenga mifumo bora ya utawala inayolenga ustawi wa wananchi wake.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.