Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mheshimiwa Atupele Mwakibete amesema serikali imekamilisha kazi ya matengenezo ya meli katika Ziwa Nyasa hivyo Mkoa wa Ruvuma sasa unaweza kufikika kwa meli,ndege na barabara.Naibu Waziri Mwakibete alikuwa anazungumza na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ofisini kwake mjini Songea baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma iliyolenga ukaguzi wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Songea ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 37 kutekeleza mradi huo.Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo amesema serikali imepata ahadi ya fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni sita kutoka SADC kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa Reli ya kutoka Mtwara hadi Mbambabay.Amesema miradi hiyo ikikamilika ukiwemo mradi wa barabara ya Morogoro hadi Ruvuma na upanuzi wa barabara ya Songea hadi Njombe,Mkoa wa Ruvuma utakuwa moja ya Mikoa yenye miundombinu bora Tanzania.https://www.youtube.com/watch?v=Gte6d295nDk
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.