MENEJIMENTI Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu Stephen Ndaki imeuagiza uongozi wa Halmashauri ya Willaya ya Nyasa kusimamia kikamlifu ujenzi wa kituo cha afya Liparamba ambao serikali imetoa shilingi milioni 500 uweze kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Akizungumza baada ya ukaguzi wa mradi huo Ndaki amesema serikali imetoa fedha za kutekeleza mradi huo muda mrefu ambapo hadi sasa bado mradi haujakamillika kwa asilimia 100 hivyo ameaagiza kasi ya kukamilisha mradi iongezwe huku akisisitiza mradi ukamillike kwa ubora na viwango vinavyolingana na thamani ya fedha.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa kwa nyakati tofauti jumla ya shilingi milioni 500 kujenga majengo ya kituo hicho ambapo katika awamu ya kwanza zilitolewa shilingi milioni 250 kujenga jengo la upasuaji na wodi ya wazazi na katika awamu ya pili zimetolewa milioni 250 kujenga jengo la wagonjwa wa nje OPD na jengo la maabara .
Mradi wa jengo la wagonjwa wa nje ambao unaendelea kutekelezwa katika kituo cha Afya Liparamba
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.