MFUKO wa Misitu Tanzania (TFF) umetoa ruzuku ya uanzishwaji wa vitalu vya miti katika shule sita zilizopo kwenye katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma.
Mafunzo hayo yametolewa na Katibu Tawala wa Mfuko wa Misitu Tanzania Dkt.Tuli Msuya, katika Ukumbi wa Oddo Mwisho mjini Mbinga ambapo amaesema ili waweze kupata ruzuku hiyo wadau lazima wawe na uwezo wa kutekeleza miradi ya uhifadhi.
Dkt Msuya amesema miradi hiyo ni chanzo cha uhakika na endelevu kwa ajili ya kugharamia, kuwezesha na uhifadhi wa maliasili ya misitu nchini Tanzania.
Shule zilizonufaika na ruzuku hiyo ni shule za msingi Masasi,Chemka,kitanda,Makunguru,Mkwaya na shule ya sekondari Mbangamao na kwamba shule hizo zitanufaika na miradi ya uanzilishwaji wa vitalu vya miti.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambaye pia ni Afisa Elimu Sekondari Stuart Kuziwa amewashukuru TFF kwa kuwajengea uwezo walimu na wanafunzi katika suala la utunzaji mazingira na kuinua uchumi kupitia miti.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.