Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Ngollo Malenya ametembelea na kukagua mradi wa maji katika kijiji cha Masuguru ambao serikali imetoa shilingi milioni 510 kutekeleza mradi huo.
Mkuu wa wilaya huyo kabla ya kufanya mkutano na wananchi wa Kijiji cha Masuguru , aliutembelea mradi huo na kujionea kazi zilizofanyika katika ujenzi wa mradi huo na kujiridhisha na kazi zilizofanyika katika kuutekeleza mradi huo wa maji.
Mhandisi David Mkondya ni Meneja kutoka wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (TARURA) amezitaja kazi zilizofanyika katika ujenzi wa mradi huo kuwa ni ujenzi wa inteki , matanki,ununuzi wa mabomba yanayotumika kulazwa kutoka kwenye chanzo mpaka kwenye matanki na ulazaji wa bomba kutoka kwenye matanki mpaka kijijini.
Mhandisi Mkondya amesema katika kijiji cha Masuguru kuna jumla ya vitongoji sita na kwamba kati ya vitongoji hivyo ni kitongoji kimoja cha Namanima ambacho hakijapata huduma ya maji kutokana na kitongoji hicho kuwa mbali zaidi ya kilomita mbili .
Hata hivyo Mkondya alifafanua kuwa kitongoji hicho kimeombewa fedha ili kichimbiwa kisima kikubwa kitakachotumika kujaza maji kwenye tanki na kisha kuwajengea vituo vya kuchotea maji wananchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.