Serikali imetoa shilingi milioni 724 kwa ajili kutekeleza miradi wa uboreshaji miundombinu ya shule za msingi na shule za awali (BOOST) katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Christopher Ngonyani wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi hiyo Julai 3, 2023.
Amesema fedha hizo zimetumika kutekeleza miradi ya BOOST katika Shule tano ambapo zimeelekezwa kwenye miundombinu ya vyumba vya madarasa, jengo la utawala, Nyumba za Walimu na matundu ya vyoo
“kati ya fedha hizo shilingi milioni 331 zinajenga Shule mpya ya mkondo mmoja shule ya msingi Kilosa iliyopo kata ya Kilosa ambapo mradi unahusisha ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa, matundu 16 ya vyoo na jengo la utawala ” alisema Ngonyani.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi Kilosa na ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Nangombo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka wasimaizi wa miradi kuifuatilia na kusimamia kikamilifu
Kanali Thomas amesema ameona dosari nyingi ambazo zimetokana nawataalamu pamoja na wasimamizi kushindwa kuja kuitembelea na kuikagua miradi hiyo mara kwa mara kwasababu wao ndio mwenye dhamana kubwa ya ufuatiliaji wa miradi ya Serikali.
Pia amewataka na kuwahimiza Wanachi kujijengea tabia ya kufutalia na kuhoji matumizi na mapato ya kila fedha ambayo Serikali imetoa kuteleza mradi kwenye maeneo yao kwani itasahidia kuziba myanya ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali na upotevu wa vifaa vya ujenzi.
“Maendeleo yanapoletwa kwenye maeneo yenu simamamieni haya maendeleo ni ya kwenu hawa wataalamu wanapita tu ila nyinyi mtabaki niwaombe simamieni hii ni miradi yenu Mhe, Rais anapowaletea miradi ioneni kama ya kwenu na wala msiruhusu wizi au mtu kualibu miradi hii” amesisitiza Kanali Thoams.
Hata hivyo amewaagiza watalaamu na wasimamizi wa miradi kuacha kuwaficha wale wote ambao wamekuwa kikwazo cha kuicheleweshaji miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za Serikali
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.