SERIKALI imetoa shilingi milioni 900 kwa ajili ya Ukarabati wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. .
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Tunduru Dr.Athuman Mkonoumo amesema ukarabati huo unaendelea kutekelezwa ambapo mpaka sasa upo hatua za mwisho.
Amesema jengo la wagonjwa wa nje OPD limekamilika kwa asilimia 70, Maabara asilimia 80 na jengo la upasuaji asilimia 95 ambapo mradi huu unatarajiwa kukamilika Novemba Mosi,2023.
Dr.Athuman Mkonoumo katika utekelezaji wa mradi huo mapaka sasa zimetumika zaidi ya shilingi milioni 816 kati ya milioni 900.
“Fedha hizi zimeletwa kama sehemu ya mpango maalumu wa Serikali wa kufanya ukarabati wa hospitali kongwe nchini na Hospitali ya Wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa hospitali kongwe nchini’’,alisema.
Amesisitiza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutapunguza changamoto kubwa ya uchakavu wa miundombinu katika Hospitali pia kusaidia kurahisisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa wilaya ya Tunduru.
Imeandikwa na Farida Baruti
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.