Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amesema Mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 ukiwepo mji wa Songea mkoani Ruvuma amepatikana.
Mheshimwa Aweso ametoa taarifa hiyo wakati anazungumza kabla ya kuzindua Bodi ya sita ya Bonde la Maji la ziwa Nyasa kwenye ukumbi wa Heritage mjini Songea.
Amesema mikataba ya mradi huo wa maji katika miji 28 nchini inatarajia kusainiwa hivi karibuni mjini Songea.
Mradi wa maji wa miji 28 nchini unatarajia kutumia zaidi ya shilingi trilioni moja fedha za mkopo wa masharti nafuu uliotolewa na Serikali ya India ili kutekeleza mradi huo.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akitoa taarifa ya miradi ya maji inayotekelezwa mkoani Ruvuma,alisema serikali inatekeleza miradi 35 mbalimbali ya maji yenye thamani ya shilingi bilioni 42.325 katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma.
Hata hivyo amesema hadi sasa miradi ya maji 45 imekamilika katika Halmashauri mbalimbali na wananchi wameanza kunufaika na miradi hiyo ya maji.
Waziri wa Maji amekamilisha ziara ya kutembelea mabonde ya maji tisa yaliyopo hapa nchini kwa kutembelea Bonde la Maji la Ziwa Nyasa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.