Mkoa wa Ruvuma umeendelea kupiga hatua kubwa katika sekta ya afya kwa kuongeza idadi ya vituo vya huduma pamoja na kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, na matumizi ya mifumo ya kielektroniki.
Hatua hizi zimeimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi, huku changamoto ya upungufu wa rasilimali watu ikibaki kuwa kipaumbele kwa mamlaka husika.
IDADI YA VITUO VYA HUDUMA ZA AFYA
Kwa sasa, Mkoa wa Ruvuma una jumla ya vituo 473 vya kutolea huduma za afya,zikiwemo Hospitali ni 18, ambapo 9 zinamilikiwa na Serikali (GoV), 7 zinamilikiwa na Mashirika ya Dini (FBO), na 2 zinamilikiwa na sekta binafsi (Private).
Vituo vya Afya ni 50, kati yake 39 ni vya Serikali, huku 11 vikimilikiwa na Mashirika ya Dini na sekta binafsi na Zahanati zipo 341, ambapo 277 zinamilikiwa na Serikali, na 64 zinamilikiwa na Mashirika ya Dini na sekta binafsi.
MATUMIZI YA MFUMO WA KIELEKTRONIKI (GoTHOMIS)
Mkoa wa Ruvuma umeendelea kusimika na kutumia mfumo wa kielektroniki wa Serikali wa GoTHOMIS katika vituo vya afya. Kufikia Januari 2024, jumla ya vituo 192 sawa na asilimia 64.74 ya vituo vyote 325 vilikuwa vimeanza kutumia mfumo huo. Lengo la mkoa ni kuhakikisha vituo vyote vimeanza kutumia mfumo huu ifikapo Desemba 2024.
HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA
Upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, na vitendanishi umeimarika kwa kiasi kikubwa katika Mkoa wa Ruvuma. Kwa mujibu wa takwimu, hali hii imeboreshwa kutoka asilimia 50 mnamo Januari 2021 hadi kufikia asilimia 84 mnamo Desemba 2024. Kuboresha upatikanaji huu kumetokana na ongezeko la mapato yanayotokana na uchangiaji wa huduma za afya, usimamizi madhubuti, na ruzuku kutoka Serikali Kuu.
Mkoa wa Ruvuma umefanya maendeleo makubwa katika sekta ya afya kwa kuongeza idadi ya vituo, kuboresha upatikanaji wa dawa, na kuimarisha mifumo ya kielektroniki
Picha ya chini ni hospitali ya Halmashauri ya Madaba wilayani Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.