MKOA wa Ruvuma hadi kufikia Mei mwaka huu una ziada ya chakula zaidi ya tani 900,000.
Hayo amesema na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme wakati anafungua kikao maaluma cha Baraza la madiwani cha kujadili ripoti ya CAG Halmashauri ya Mbinga,kilichofanyika ukumbi wa Benjamini Mkapa katika shule ya sekondari Kigonsera .
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa hadi kufikia Mei 15 mwaka huu Mkoa ulikuwa umevuna zaidi ya tani milioni 1.4 za mazao ya chakula na biashara.
‘’Tunamshukuru Mungu ametupa Mvua nzuri na ametuepusha na wadudu wa haribifu hivyo tunatarajia kuvuna mazao mengi mwaka huu katika Mkoa wetu’’.
Hata hivyo Mndeme ametoa raia kwa wakulima wajiepushe kuuza mahindi kwa bei ndogo kwa sababu mahitaji ya chakula mwaka huu ni Makubwa na kwamba walanguzi wananunua kwa bei ndogo hivyo wasifanye haraka kuuza.
Ametoa rai kwa wakulima kusubiri serikali itoe bei nzuri ili wananchi waweze kupata faida badala ya kunyonywa na walanguzi ambao hivi sasa wapo wengi wanapita kwa wakulima ili kununua mazao kwa bei ndogo.
Mkoa wa Ruvuma katika msimu wa 2018/2019 ulioongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula nchini kwa kuzalisha jumla ya tani 1,166,816.
IMEANDIKWA NA ANET NDONDE
OFISI YA HABARI YA MKOA WA RUVUMA
JUNI 2,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.