Mkoa wa Ruvuma umeendelea kufanya vizuri katika sekta ya kilimo, ambapo kwa msimu wa kilimo wa 2023/24 umezalisha tani milioni 1,955,763.76 za mazao ya chakula.
Akizungumza kwenye kikao cha Kamati cha Ushauri RCC Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema Mahitaji halisi ya mkoa ni tani 470,000, hivyo kusababisha ziada ya tani milioni 1,485,763.76 ambazo huuzwa ndani na nje ya mkoa, hali inayowaongezea wananchi kipato.
Ameyataja Mafanikio haya yanatokana na mfumo wa pembejeo za ruzuku ya mbolea na mbegu unaotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ameongeza kuwa Mpango huo umewezesha wakulima kupata pembejeo kwa gharama nafuu, hivyo kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya chakula.
Kwa msimu wa kilimo wa 2023/24, Mkoa wa Ruvuma umetumia tani 113,000 za mbolea. na kwamba kwa msimu wa 2024/25 hadi kufikia Januari, tayari tani 55,488.886 za mbolea zimekwishatumika.
Matumizi haya makubwa ya pembejeo yamechangia ongezeko la uzalishaji wa mazao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.