Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema hadi kufikia Oktoba 17 2024,Mkoa wa Ruvuma umefikia asilimia 60.7 ya wananchi waliojiandikisha katika daftari la mpiga kura.
Kanali Abbas amesema hayo baada ya kupokea taarifa ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwenye ukumbi Bishop Mwalunyungu mjini Tunduru.
Amesema hali ya uandikishaji katika daftari la mpigakura katika Mkoa wa Ruvuma inaendelea vema ambapo Waziri mwenye dhamana ya TAMISEMI ameutangaza Mkoa wa Ruvuma Umeshika nafasi ya pili kitaifa kwa uandikishaji wa awali wa daftari la mpigakura.
“Matokeo hayo yanaonesha kazi kubwa ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha imefanyika ,hata hivyo kwa takwimu hizi msibweteke kwa sababu zimebaki siku chache,lengo ni kufika uandikishaji kwa asilimia 100’’,alisisitiza.
Awali Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Chiza Marando alisema hadi kufikia Oktoba 16,2024 jumla ya walijiandikisha katika daftari la wapigakura walifikia 131,042 sawa na asilimia 53.8.
Amesema kati ya waliojiandikisha wanaume ni 62,104 na wanawake ni 68,938 na kwamba Halmashauri hiyo imelenga kuandikisha wapigakura wapatao 243,364 kati yao wanaume 117,199 na wanawake 126,165.
Hata hivyo Marando amesema timu ya hasama katika Halmashauri hiyo imendelea kutoa elimu kwa jamii,kuhamaisha wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kupitia matangazo ya redio,matangazo ya magari,vipeperushi,mabango na elimu ya nyumba kwa nyumba.
Zoezi la uandikishaji wapigakura kwa maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa linafanyika kwa siku kumi nchini kote kuanzia Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.