Wananchi wa Kata ya Mkongo Gulioni, Kijiji cha Mkongo, wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa shilingi milioni 224 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa nane na matundu 14 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Kimolo.
Ujenzi huu umeleta matumaini mapya kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.Mradi huu umeongeza miundombinu ya shule na kuongeza nafasi kwa wanafunzi zaidi ya 350, ambao sasa wanapata mazingira bora ya kusomea.
Wananchi na viongozi wa eneo hilo wamesifu jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu, hususan maeneo ya vijijini ambako changamoto za miundombinu ya shule zimekuwa kubwa kwa muda mrefu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Ndugu Philemon Mwita Magesa, amepongezwa kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.