Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imekabidhi mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 313,350,550 kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Simon Chacha. ambaye amesema Mikopo hiyo ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya halmashauri inayotolewa kwa vikundi maalum ili kuwawezesha kiuchumi.
, Mheshimiwa Chacha alisisitiza umuhimu wa mikopo hiyo katika kuboresha maisha ya wananchi na kusaidia juhudi za serikali za kupunguza umaskini.
Aliwataka wanufaika kuhakikisha wanatumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kurejesha mikopo kwa wakati ili wengine pia waweze kunufaika.
“Mikopo hii ni fursa muhimu kwa wananchi kuongeza kipato na kuboresha maisha yao. Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunaitumia vyema ili kuleta maendeleo katika wilaya yetu,” alisema Mheshimiwa Chacha.
Aliongeza kuwa serikali imeweka mfumo mzuri wa utoaji wa mikopo, hivyo ni wajibu wa wanufaika kurejesha fedha hizo kwa wakati.
, Mheshimiwa Chacha alimwagiza Afisa Maendeleo ya Jamii kuwasaidia wananchi kutambua miradi isiyokidhi vigezo vya mikopo mapema.
Amesisitiza hatua hiyo itasaidia kuzuia wananchi kutumia gharama kubwa kuanzisha mchakato wa maombi ya mikopo kwa miradi isiyo na sifa za kukopesheka.
Mikopo hii inalenga kuwawezesha kiuchumi wanufaika kwa kuwasaidia kuanzisha au kukuza biashara zao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.