Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas anaendelea na ziara ya kikazi na kukutana na makundi mbalimbali ili kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Hapa Mkuu wa Mkoa amekutana na makundi matatu ya wajasiriamali wadogo ambao ni wafanyabiashara wadogo (Wamachinga),madereva bajaji na madereva boda boda kwenye kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Wajasiriamali hao wamemweleza Mkuu wa Mkoa kero mbalimbali zikiwemo za ubovu wa miundombinu ya masoko ya Songea,changamoto za maeneo ya kuegeshea bajaji na changamoto ya miundombinu ya barabara za Manispaa ya Songea.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.