Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas kesho Februari 23,2023 anatarajia kuzindua wiki ya kumbukizi ya miaka 117 ya mashujaa wa vita ya Majimaji ambayo kilele chake ni Februari 27,2023.Uzinduzi huo unafanyika kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Mahenge mjini Songea.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Mhifadhi Bartazar Nyamusya anasema tamasha hili hufanyika kila mwaka kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Februari 25 hadi Februari 27 ambayo ni siku ya kilele.
“Tamasha lilianza kuratibiwa na Makumbusho ya Taifa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya Utalii na Utamaduni, Taasisi za elimu vikiwemo Vyuo Vikuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Vyombo vya Habari na Mashirika ya Umma na watu binafsi’’,anasisitiza.
Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho ya Taifa Philipo Maligisu ameyataja malengo ya kufanyika kumbukizi la vita ya majimaji kila mwaka kuwa ni Kutangaza zaidi Tamasha la Utalii wa Utamaduni Ndani na Nje ya nchi ili kuendana na sera ya Utalii ya 2009,sera ya Utamaduni ya 1997 na Sera ya MaliKale ya 2008.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.