MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas atakuwa mgeni rasmi katika Ibada ya Kitaifa ya Ijumaa Kuu ambayo kitaifa inafanyika leo Ijumaa Kuu Aprili 7,2023 kuanza saa 8.30 mchana katika Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi la KIUMA wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Hata hivyo katika Ibada hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Wakili Julius Mtatiro atamwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas .
Kanali Thomas anawatakia wakristo na wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma Ibada njema ya Ijumaa Kuu inayofanyika ulimwenguni kote.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Mkoa wa Ruvuma Askofu Raphael Haule amesema,Ibada ya Ijumaa Kuu kitaifa itakuwa mubashara kupitia TBC kutoka kanisa la Upendo wa Kristo Masihi KIUMA wilayani Tunduru.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.