Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngolo Malenya, amezindua gari jipya la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani humo.
Hatua hiyo nayolenga kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya chama na kuboresha huduma kwa wanachama wake.
Uzinduzi huo umefanyika katika hafla maalum ambapo Malenya aliipongeza CWT kwa juhudi zake za kuhakikisha walimu wanapata usafiri wa uhakika.
Amehimiza viongozi wa chama hicho kutunza gari hilo ili lidumu kwa muda mrefu na kusaidia katika utekelezaji wa shughuli za walimu na jamii kwa ujumla.
Malenya pia amewataka waajiri kuhakikisha madereva wanaoajiriwa wana sifa stahiki na wanazingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali zisizotarajiwa.
Kwa upande wake, Katibu wa CWT Wilaya ya Namtumbo, Deograsias Haule, amesema gari hilo limegharimu shilingi milioni 77, ikijumuisha gharama za ununuzi, marekebisho, na bima.
Ameeleza kuwa awali walikabiliwa na changamoto ya usafiri, hasa wanapohitaji msaada wa dharura, lakini sasa changamoto hizo zitapungua.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CWT Taifa anayewakilisha Mkoa wa Ruvuma, Sabina Lipukila, amesema chama kimejikita katika kutatua changamoto za usafiri kwa walimu.
Wilaya nne kati ya tano za mkoa huo tayari zimenunua mabasi, huku nyingine zikiendelea na mchakato wa ununuzi ili kuhakikisha walimu wanapata usafiri wa uhakika kwa shughuli zao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.