SERIKALI kupitia Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 5.5 kujenga mradi wa Maji Kata ya Mtiyangimbole Halmashauri ya Madaba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa na Meneja wa RUWASA Wilaya ya Songea Mhandisi Mathias Pangras wakati anatoa taarifa ya mradi huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Kapenjama Ndile alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua mradi huo.
Mhandisi Mathias amesema ujenzi wa Mradi huo ulianza Novemba 25,2022 na unatarajia kukamilika Novemba 25 mwaka huu.
Amesema mradi huo ukikamilika utahudumia wakazi 11,239 katika Vijiji vitatu katika Kata ya Mtyangimbole.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo,Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile ametoa rai kwa Mkandarasi Names Corporate.Co.Ltd kuhakikisha anakamilisha mradi huo ndani ya mkataba ili uweze kuwahudumia wananchi ambao wanahitaji maji safi na salama.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.