MSAJILI wa Hati Msaidizi wa Mkoa wa Ruvuma Christina Nyerere ametoa wito kwa Wananchi ambao waliwai kusajili hati kabla ya kuanzishwa kwa ofisi za mikoa, kuwa hati hizo bado zipo ofisini na amewataka watembelee ofisi ya Aridhi Mkoa kuzichukua
Hayo ameyazungumza wakati wa kikao cha watumishi wa Sekta ya Aridhi Mkoa wa Ruvuma ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea kilichofunguliwa na kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Jeremiah Sendoro Machi 21, 2023.
Christina amesema kwa sasa muitikio ni mkubwa sana kwa Mkoa wa Ruvuma kwani Wananchi wameanza kuamka kwa sababbu moja wa maelekezo kutoka Wizara ya Aridhi ni kufanya semina na kutembelea wajumbe kuwaeleza ofisi zipo na wanatoa huduma gani
“Kama mtu anafahamu anakiwanja chake na aliwahi kuomba hati tunamshauri atembelee ofisi ya Aridhi Mkoa aje kuchukuwa hati yake”
Pia ameeleza hadi sasa hati zilizo sajiliwa kwa mwaka huu wa fedha 22/23 ni jumla ya hati 939 na zilizochukuliwa hadi sasa takribani ya hati 800 kwa sababu wanaendelea kusajili
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.