Mwenge wa Uhuru 2024 umehitimisha mbio zake mkoani Ruvuma kwa kukagua miradi katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.
Akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2024 kuhusu mradi wa ujenzi wa maji katika Kijiji cha Mbangamawe Halmashauri ya Madaba,Meneja wa RUWASA Wilaya ya Songea Mhandisi Mathias Charles amesema RUWASA ilipokea Zaidi ya shilingi milioni 545 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji hicho.
Amesema utekelezaji wa mradi huo umehusisha ujenzi wa tanki lenye uja zo wa lita 50,000,ujenzi wa banio la maji,ujenzi wa sampu tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 30,000,nyumba ya mtambo,chumba cha mlinzi,choo na vituo sita vya kuchotea maji .
Amesema mradi huo una faida mbalimbali zikiwemo wananchi wapatao 2,800 kunufaika na upatikanaji wa huduma ya maji na salama hivyo kupunguza umbali wa kufuata maji.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Madaba umeweka jiwe la msingi ujenzi mradi wa lami nyepesi barabara ya Kifaguro-Magingo yenye urefu wa kilometa 5.6
Mradi huo unatekelezwa na TARURA kwa gharama ya Zaidi ya shilingi milioni 563 ambapo kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo,kutarahisisha wananchi wa Halmashauri hiyo kufika kwa urahisi katika jengo la Makao makuu ya Halmashauri, hospitali ya Wilaya,shule ya msingi Kifaguro na sekondari ya Madaba hivyo kupata huduma za kijamii kwa urahisi.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Madaba pia umekagua mradi wa upandaji miti katika uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji hifadhi ya Wino ambayo ina ukubwa wa hekta 39,718,Msitu huo unaoundwa na safu tatu za Wino,Ifinga na Mkongotema.
Hifadhi ya Msitu wa Wino inaendelea na uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji na kuvitumia katika shughuli za uzalishaji wa miche ya kupanda na matumizi ya majumbani.
Miongoni mwa vyanzo vya maji muhimu vinavyoendelea kulindwa ni Igawisenga, Mgombezi, Mwendesi na Kibanditi ambapo wananchi wamepanda miti 20,000 itakayosaidia kutunza vyanzo vya maji,kuimarisha kilimo cha zao la nyuki na kupanda matunda mbalimbali.
Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Madaba umeweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la Lituta linalogharimu Zaidi ya shilingi milioni 190 na kwamba kukamilika kwa mradi huo kutaongeza mapato katika Kijiji na kuboreshwa mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava amekagua na kuzindua vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Ngadinda ambapo jumla ya shilingi milioni 53 zimetumika kutekeleza mradi huo.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Madaba ulisomewa taarifa ya ugawaji wa vyandarua kwa akinamama wajawazito na Watoto chini ya mwaka mmoja ambapo katika kipindi cha Julai 2023 had Mei 2024 Halmashauri hiyo ilipokea vyandarua 5040 vyenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 36
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.