KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2022 Ndugu Sahil Nyanzabara Geraruma amekagua Miradi minne na kuzindua Miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Milioni 560.5 Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi na ukaguzi huo amepongeza usimamizi wa Miradi na kuwataka viongozi wa Wilaya ya Namtumbo kuendelea kusimamia Miradi hiyo ya Serikali.
Ndugu Sahili Geraruma amekagua vibanda vya vikindi vinavyojihusisha na huduma ya utoaji elimu ya lishe kwa jamii, amekagua klabu ya wanafunzi ya kupinga rushwa katika shule ya sekondari Nasuli, amekaguac chanzo cha chemichemi ya maji kilichoifadhiwa katika kijiji cha Luegu pamoja na kukagua Mradi wa uwezeshaji vijana wa mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti kijiji cha Mkongo mwinuko.
Pia amezindua Mradi wa ujenzi wa madarasa manne katika shule ya sekondari Nanungu, amezindua kiwanda cha kuchakata mazao, amezindua zoezi la ugawaji wa vyandarua kwa akina mama wajawazito na wenye watoto wachanga, amezindua zoezi la uwekaji anwani za makazi na postikodi pamoja na uzinduzi wa nyumba ya kulala wageni katika kijiji cha Nyalamatata.
“Ndugu wananchi Mwenge wa Uhuru umekua ni kichocheo kikubwa cha maendeleo na unaendelea kutuhamasisha juu ya kudumisha amani na upendo”, amesema Sahil Geraruma.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Kenneth Ningu amemshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa kuukimbiza mwenge Wilaya ya Namtumbo salama pia amehaidi kutekeleza maagizo aliyopewa na kuendelea kutimiza majukumu ya Serikali .
Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Namtumbo umekimbizwa umbali wa Kilomita 217 na kupita katika kata 11 kati ya kata 21 za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo tarehe 14 Aprili 2022.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 “Sensa ni Msingi wa mipango ya maendeleo shiriki kuhesabiwa tuyafikie malengo ya Taifa”.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Aprili 19 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.