Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, amewataka wananchi kushirikiana na viongozi wa chama kupinga vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wanaotaka madaraka kwa njia zisizo halali.
Akizungumza katika kata za Luhangarasi na Upolo, wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma, Komred Mwisho amelaani tabia ya wagombea kutoa rushwa kwa wananchi ili wapate nafasi za uongozi, akisisitiza kuwa ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha uongozi wa chama unasimamiwa kwa haki na uwazi.
Mwisho ametoa shukrani kwa wananchi baada ya vitongoji vya kata hizo kuibuka na ushindi mnono kupitia CCM, akisema ushindi huo ni kielelezo cha imani yao kwa chama.
Pia amewapongeza viongozi wa kata ya Luhangarasi kwa kushinda uchaguzi katika vitongoji vyote kupitia CCM.
Amewasihi viongozi hao kuwa waadilifu na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa uaminifu ili kuendeleza maendeleo ya wananchi waliowachagua. Aidha, amewahimiza wananchi waendelee kuwa na imani na CCM kwa sababu chama hicho kimekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza ilani yake.
Amesema maendeleo yanayoonekana sasa, yakiwemo umeme, maji safi na ujenzi wa barabara, ni matokeo ya utekelezaji wa ilani ya CCM chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.