MKUU wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngollo Malenya amesema wilaya ya Namtumbo inatarajia kufanya tamasha la siku mbili la utalii na uwekezaji kuanzia Septemba 22 hadi 23 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe .
Malenya amesema tamasha hilo limepewa jina la Namtumbo Kihenge na amelitaja lengo la tamasha hilo ni kutangaza fursa za uwekezaji kwenye maeneo ya kilimo,madini pamoja na kuhamasisha watalii kuja kutembelea Namtumbo.
Aidha Malenya amebainisha kuwa tamasha hilo litawakutanisha watu mbalimbali Ili waweze kuitambua Namtumbo pamoja na fursa zake zilizomo.
Mratibu wa Tamasha hlo Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Perez Kamugisha alisema tamasha Hilo limepewa jina la Namtumbo Kihenge Kumaanisha mchango wa wilaya ya Namtumbo katika ghala la hifadhi ya chakula la taifa.
Kamugisha alifafanua kuwa Mkoa wa Ruvuma unaongoza kitaifa katika kuzalisha mazao ya chakula huku wilaya ya Namtumbo ikiongoza katika kuzalisha katika Mkoa wa Ruvuma na kufanya wilaya ya Namtumbo kuchangia katika hifadhi ya chakula katika ghala la taifa.
Hata hivyo Kamugisha amesema Kihenge ni ghala lililotengenezwa Kwa kutumia mianzi na kusiribwa udongo kisha kutumiwa na wakulima kuhifadhia mazao Kwa ajili ya kuweka akiba ya chakula.
Pamoja na hayo Kamugisha alibainisha mambo yatakayofanyika katika tamasha Hilo ni pamoja na kuendesha baiskeli za milimani ,kutakuwa na marathon iliyopewa jina la Namtumbo Kihenge Marathon pamoja na kuwa na mkutano na wadau mbalimbali wa biashara za kilimo,madini na kuwavutia watu mbalimbali kuja kufanya utalii wilayani Namtumbo kutokana na kuwepo Kwa geti la utalii la Mwalimu Nyerere pamoja na kumsaidia Mheshimiwa Raisi kutangaza utalii kupitia video vya Royal toure.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.