• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

NAMTUMBO yaagizwa kuongeza kasi ya kushughulikia hoja za CAG

Imewekwa kuanzia tarehe: June 15th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kuongeza kasi ya kushughulikia hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), licha ya halmashauri hiyo kupata hati safi.

Akizungumza katika Baraza Maalum la Kujadili Hoja za CAG kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Namtumbo, Kanali Ahmed alisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi katika utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na CAG.

“Nimesikia hapa kulikuwa na hoja 27, kati ya hizo ni 7 tu ndizo zimefanyiwa kazi na kufungwa, 20 zipo kwenye utekelezaji. Hii kasi ya kushughulikia hoja ni ndogo, mnahitajika kuongeza bidii, umakini na uharaka wa utekelezaji," alisema Kanali Ahmed.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Phiniel Mbula, alibainisha kuwa ofisi ya mkoa inatoa vyeti kwa watumishi waliosaidia upatikanaji wa hati safi.

Alilitaja lengo  la kutoa vyeti hivyo ni kutambua mchango wa wafanyakazi, mkurugenzi, madiwani na sekretarieti ya mkoa, ambao wamesimamia vyema taratibu za kifedha, uadilifu na uzalendo.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Namtumbo, Fransis Mgoloka, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, aliipongeza halmashauri kwa mafanikio yaliyopatikana. Aliahidi kuendelea kufuatilia na kusimamia hoja zilizosalia, ili hatimaye zifungiwe na halmashauri ipate alama ya juu ya uwajibikaji.

Kanali Ahmed alihitimisha kwa kusisitiza kuwa usimamizi wa fedha za umma si lele mama, bali ni wajibu wa kisheria na kimaadili.

 Alivitaka vyombo vyote vinavyohusika kuhakikisha hoja za CAG zinafanyiwa kazi kwa wakati, ili halmashauri iendelee kutoa huduma bora kwa wananchi.


Hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuagiza Halmashauri ya Namtumbo kuongeza kasi ya kushughulikia hoja za CAG ni ishara ya uongozi makini unaojali uwazi, uadilifu na uwajibikaji.

Ni wito kwa watumishi wa umma, madiwani na wadau wote kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika vizuri, hoja zinafungwa, na hatimaye huduma bora zinamfikia mwananchi wa kawaida.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WAKULIMA Ruvuma waomba soko la mahindi kufunguliwa haraka

    June 16, 2025
  • SERIKALI ,dini na wananchi Ruvuma waungana kudumisha amani

    June 16, 2025
  • RUVUMA yaandika historia chupa 4040 za damu zakusanywa kuokoa maisha

    June 15, 2025
  • NAMTUMBO yaagizwa kuongeza kasi ya kushughulikia hoja za CAG

    June 15, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.