SERIKALI imeidhinisha zaidi ya shilingi bilioni kumi kwa ajili ya kutekeleza shughuli za mendeleo katika Halmashauri ya Nyasa mkoani Ruvuma katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Ndugu Khalid Khalif wakati anazungumza na wanahabari ofisini kwake Kilosa mjini Mbambabay.
Amesema kati ya fedha hizo zaidi ya shilingi bilioni 4.1 ni fedha za ndani na zaidi ya shilngi bilioni 5.9 ni fedha za nje na kwamba kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri hiyo imepokea zaidi ya shilingi bilioni 7.9 sawa na asilimia 78.6 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 3.3 fedha za ndani.
“Halmashauri pia imepokea zaidi ya shilingi bilioni 4.5 fedha za nje na zaidi ya shilingi milioni 319,fedha zilizotolewa nje ya bajeti hivyo kufanya mapokezi ya fedha zote kuwa ni zaidi ya shilingi bilioni 8.2’’,alisema Khalif.
Hata hivyo amesema hadi kufikia Juni 30 mwaka huu zaidi ya shilingi bilioni 6.6 zilikuwa zimetumika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo sawa na asilimia 80 ya fedha zilizopokelewa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyasa Mheshimiwa Sterwat Nombo amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 2.9 kutekeleza mradi wa jengo la ofisi ya Mkrugenzi wa Halmashauri ya Nyasa ambapo hivi sasa watalaam wanafanya kazi vizuri ya kuwahudumia wananchi.
Amesema serikali hadi sasa imetoa shilingi bilioni 3.3 kuboresha miundombinu ya afya katika hospitali ya wilaya ya Nyasa ambapo hivi sasa wananchi wanapata huduma zote muhimu ndani ya wilaya.
Amesisitiza kuwa miaka mitatu ya Rais Samia imeleta faraja kubwa kwa wananchi wa Nyasa na kwamba kumekuwa na mafuriko ya miradi ya mabilioni ya fedha iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma ambayo inapakana na nchi za Malawi na Msumbiji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.