MKUU wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Ngollo Malenya amesema geti la Hifadhi ya Taifa ya Nyerere katika Wilaya ya Namtumbo linafunguliwa rasmi Septemba 22,2023 na wananchi wataanza kufanya utalii katika hifadhi ya Nyerere inayoongoza kwa ukubwa barani Afrika.
Amesema ufunguzi wa geti hilo ni sehemu ya tamasha la kutangaza fursa mbalimbali zilizopo Wilayani Namtumbo na kwamba tamasha hilo limepewa jina la Namtumbo Kihenge ambalo linafanyika kwa siku mbili kuanzia Septemba 22 hadi 23 ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.