Programu ya Uwezeshaji Wananchi kiuchumi inayoitwa Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) imezinduliwa mkoani Ruvuma kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Uzinduzi huo umehusisha mkutano wa viongozi wa Mkoa,wakuu wa Wilaya,Makatibu Tawala wa Wilaya,waratibu wa uwezeshaji ngazi ya Mkoa na Halmashauri na viongozi wa majukwaa ya uwekezaji wanawake kiuchumi wa Halmashauri zote.
Programu hiyo pia imehusisha mkutano wa wajasiriamali wote Pamoja na viongozi,mkutano ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa parokia ya Bombambili mjini Songea.
Akizungumza kwenye nyakati tofauti kwenye Uzunduzi huo katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na ukumbi wa Parokia ya Bombambili, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bibi Beng’i Issa amesema IMASA ni programu ambayo inatekelezwa katika mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.
Amelitaja lengo kuwa la IMASA kuwa ni kuimarisha uchumi wa wananchi na kwamba Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linasimamia Programu hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo amewataja watekelezaji wakubwa wa programu hiyo ni Mkuu wa Mkoa ,Mkuu wa wilaya na Halmashauri zote.
Hata hivyo amesema IMASA imebuniwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Ikulu ambapo Baraza la Uwezeshaji linafanya kazi kwa kushirikiana na Mshauri wa Rais ambaye anashughulikia masuala ya wanawake,Vijana na Makundi Maalum.
“IMASA ni matakwa na maoni ya Mheshimiwa Rais,ambaye amedhamiria kuwasaidia wananchi kwa kupitia Ofisi za wakuu wa mikoa’’,alisema.
Hata hivyo amesema program hiyo itatekelezwa katika awamu mbili,ambapo katika awamu ya kwanza zinahitajika takwimu za wananchi waliopo mkoani Ruvuma na mikoa mingine ambapo unatumika mfumo wa kidigitali ambao utamwezesha mwananchi mwenyewe kuingiza taarifa zake zote muhimu.
Amesema wananchi wakati wanaingiza taarifa zao zitakuwa zinaonekana moja kwa moja kwenye mfumo hivyo kuonesha idadi kamili ya watu waliojisajiri ambapo amesema uzinduzi unaofanyika Ruvuma umefikisha mikoa nane hadi sasa iliyopitiwa na IMASA.
Amesema katika Mkoa wa Ruvuma usajiri utafanyika kwa wiki mbili kwenye mfumo ambapo baada ya zoezi hili itatengezwa program maalum kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ambao ni wanawake,vijana na wenye mahitaji maalum.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Peres Magiri ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi kujisajiri kwenye mfumo.
Amesisitiza kuwa mfumo huo utawezesha upatikanaji wa kanzidata na taarifa mbalimbali za makundi na watu binafsi wanaojihusisha na kazi mbalimbali za kiuchumi ili waweze kuwezeshwa kiuchumi kupitia IMASA.
Ameutaja Mkoa wa Ruvuma kuwa wananchi wake wanajishughulisha na kazi mbalimbali za kuchumi zikiwemo kilimo,uchimbaji madini,uvuvi,ufugaji na usindikaji wa bidhaa mbalimbali.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Viwanda,Uwekezaji na Biashara Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Martin Kabaro amesema katika kipindi cha mwaka 2021/2022 serikali ilitoa mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 2.56 kwa vikundi 327 vya wanawake,vijana na wenye ulemavu.
Amesema serikali pia ilitoa mikopo ya Zaidi ya shilingi bilioni 1.3 kwa vikundi 164 vya wanawake,vijana na wenye ulemavu hadi kufikia Machi 2023.
Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma Januari 2024 umepokea mashine 20 za kukamua alizeti zilizonunuliwa kwa ajili ya vikundi 20 vilivyopo katika Halmashauri za Ruvuma.
Wajasirimali wadogo wakiwa kwenye mafunzo ya Programu ya Imarisha Uchumi na Mama Samia kwenye ukumbi wa Parokia ya Bombambili mjini Songea
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.