Mataifa zaidi ya 30 yanashiriki maonesho ya kimataifa ya kilimo maarufu nanenane mwaka 2023 yanayofanyika kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya kuanzia Julai 25 hadi Agosti 8.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wakuu wa mikoa ya Songwe, Katavi, Rukwa, Ruvuma,Iringa na Njombe inayounda kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Juma Homera amesema kutokana na umuhimu wa maonesho hayo kumekupo na ongezeko la nchi kutoka 11 za awali kufikia zaidi ya nchi 30.
Mh.Juma Homera ameongeza kuwa maonesho ya mwaka huu yanabebwa na kaulimbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu wa chakula” ikiwa ni muelekeo wa mkutano wa jukwaa la mifumo ya chakula Afrika (Africa food Forum) 2023 utakaofanyika tarehe 5 hadi 8 Septemba,2023 Jijini Dar es salaam.
Homera ameeleza kuwa maonesho ya kimataifa ya Kilimo mwaka huu yaliyofunguliwa na Mh.Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdory Mpango Agosti Mosi yanatarajiwa kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Agosti nane,2023 ambayo ni siku ya Kilele.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.