RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi bilioni 223 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Wakili Julius Mtatiro amesema fedha hizo zimetolewa katika kipindi cha Machi 2021 hadi Machi 2023,
DC Mtatiro ameeleza kuwa mradi wa kipekee na kihistoria ambao umetia fora ni ule wa Shilingi Bilioni 150 ambazo zimepelekwa wilayani humo kukamilisha ujenzi wa Msongo Mkubwa wa umeme wa kilovoti 220 kutoka Songea hadi Tunduru wenye utefu wa kilomita 210, mradi ambao utamaliza kabisa matatizo ya umeme wilayani Tunduru na ambao utakamilika ndani ya miezi 15 huku Wakandarasi wakiwa wamesharipoti wilayani humo.
Miradi mingine iliyopeleka fedha nyingi wilayani Tunduru ni REA Shilingi Bilioni 31.9, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Shilingi Bilioni 9.6, Barabara Vijijini Shilingi Bilioni 8, Miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari Shilingi Bilioni 7.4, Miundombinu ya Sekta ya Afya Shilingi Bilioni 3.1, Miundombinu ya Maji Shilingi Bilioni 5.2, Kilimo na Ushirika Bilioni 4.5, Elimu Bila Malipo Shilingi Bilioni 1.5.
DC Mtatiro amewaasa wananchi wa Tunduru kuitunza miundombinu yote inayojengwa katika Wilaya hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.