Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekabidhi zawadi kwa watoto yatima kuelekea Sikukuu ya Iddi.
Zawadi hizo zimetolewa kwa vituo vitatu vilivyopo Wilayani Songea ambavyo ni Good Shepherd Orphanage, St. Antony na kituo cha wahitaji wanaohudumiwa na BAKWATA mkoa wa Ruvuma.
Akikadidhi zawadi hizo, Kanali Ahmed amesema zawadi hizo zimegharimu shilingi milioni 1,845,000 ambapo kila kituo kimepata mbuzi mmoja, mchele kilo 50, sukari kilo 25, mafuta ya kupikia lita 10, mfuko mmoja wa sabuni, na katoni 10 za juisi.
Amesema zawadi hizo zimetolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia kwa ajili ya kuwashika mkono watoto yatima kuelekea sikukuu ya iddi na wale wanaoendelea na Kwaresma.
Baada ya kupokea zawadi hizo, Sheikh wa Mkoa wa Ruvuma, Ramadhani Mwakilima, amethibitisha kupokea zawadi hizo na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa zawadi hizo ambazo zinaenda kuwa faraja kubwa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.