. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Zawadi za sikukuu zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1.8 kwa vituo vitatu vya kulelea watoto yatima katika Wilaya ya Songea.
Zawadi hizo zimekabidhiwa katika vituo hivyo kwa niaba ya Rais na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed kwenye hafla fupi iliyofanyika katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Good Shepherd Orphanage kilichopo Mjimwema Manispaa ya Songea.
Vituo vingine vilivyokabidhiwa zawadi hizo ni St. Antony na Wahitaji wanaohudumiwa na BAKWATA Mkoa
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Machi 31,2025 atakula chakula na watoto yatima 300 kutoka katika vituo vya kulelea yatima kutoka wilaya Zote za Mkoa wa Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.