RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amewaagiza wakuu wa mikoa nchini hasa yenye mito na vyanzo vya maji inayopeleka maji Bwawa la Julius Nyerere kuwaondoa watu wote waliovamia maeneo ya mito hiyo ukiwemo mto wa Ruaha Mkuu.
Amesisitiza suala la kulinda mito na vyanzo vya maji ni la kufa na kupona huku akisema hakuna mkubwa aliyekuwa juu ya sheria hivyo watu wote waondolewe haraka na wakuu wa mikoa wasimamie hilo.
Rais Dk.Samia ametoa maelekezo hay oleo Desemba 22,2022 baada ya kubonyeza kitufe cha kuashiria kuanza kujaza maji kwenye Bwawa la Julius Nyerere ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 78.68.Tukio hilo limeshuhudiwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi.
“Mradi huu umetumia fedha nyingi sana, hivyo kulinda vyanzo vya maji vya mto Rufiji sasa ni kufa , kupona.Mto Ruaha Mkuu utachangia maji kwenye bwawa hili kwa asilimia 15 , hivyo niwaombe watu wa Iringa na Mbeya kuachana na yale wanayofanya kule ili maji yatitirike
“Mto Kilombero utachangia maji asilimia 65 , Mto Luega utachangia asilimia 15, hivyo niwaombe wananchi wa Morogoro na Iringa watunze vyanzo vya maji, lakini mto Rufiji pia unachangiwa maji na vimito vidogo vidogo hivyo lazima tulinde.”
Rais Samia amesema mifugo yote iliyongia kinyume na utaratibu kwenye maeneo ya vyanzo vya maji hasa katika mito hiyo ikaondolewe.“Kwa mifugo ambayo itakayongia kwenye vijiji, lazima uwezo wa vijiji hivyo uangaliwe sio tu kuingiza mifugo.”
Aidha amesema wanapokwenda kuhamisha ni vema sheria, kanuni na taratibu zikafuatwa.
“Mkoa wa Morogoro katika Wilaya ya Kilosa migogoro ya ardhi ni mingi kutokana na mifugo inayoingia kule Kilosa.Hakuna mkubwa atakayetuharibia vyanzo vya maji, wakuu wa mikoa waende wakatekeleza wajibu wao na kama kuna wakuu wa mikoa wanaogopa wakubwa basi wanyooshe mkono ili wakubwa wawashughulikiwe.”
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.