MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed pichani kushoto,amefunga Bonanza la Eid El Fitr ambalo lilikuwa linafanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo Timu ya soka ya Kazaroho imeibuka washindi kwenye Bonanza hilo baada ya kuifungua timu ya Songea kwanza bao moja kwa bila na kuweza kujinyakulia kombe na kujipatia kitita cha fedha taslimu shilingi 500,000
Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa pamoja na wadau wengine wa michezo wakifuatilia mchezo wa soka fainali kati ya Timu ya Kazamoyo na Songea kwanza kwenye uwanja wa michezo wa Majimaji ambako timu ya Kazaroho ilibuka mshindi na kuchukua kikombe na fedha taslimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.