RC RUVUMA ASISITIZA KUFANYIWA KAZI USHOROBA WA SELOUS-NIASSA
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesisitiza kuendelea kufanyiwa kazi kwa ushoroba wa Selous -Niassa ili kudhibiti muingiliano wa Wanyamapori wasilete madhara makubwa kwa Wananchi.
Kanali Ahmed ameyasema hayo alipokuwa akizindua mradi wa Global Biodiversity Framework, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Hunt Club Mjini Songea, Mkoani Ruvuma.
"Niendelee kusisitiza ushoroba huu wa Selous pamoja na Niassa ambao ni muunganiko mzuri baina yetu na Msumbiji, tuendelee kuufanyia kazi ili kudhibiti muingiliano wa Wanyamapori na Wanadamu ili wasilete madhara makubwa",Alisema.
Sanjari na hayo ameeleza jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhakikisha Wanyamapori hawaleti madhara makubwa kwa nchi ikiwemo utoaji wa elimu, kufanya doria kwenye maeneo hatarishi, kuendelea kuwaandaa Askari Wanyamapori wa vijijini pamoja na kutumia ndege nyuki.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Uifadhi wa Mazingira na Wanyamapori Duniani (WWF) Tanzania Dkt. Amani Ngusaru amebainisha Kusifika Kwa Tanzania Kikanda na Kimataifa kama Nchi yenye utajiri mkubwa wa bio-anuai.
Amesema Tanzania imetenga takribani asilimia 40 ya ardhi yake kwa ajiri ya uifadhi wa maliasili, misitu na Wanyamapori na kutokana na hilo Tanzania ni mojawapo ya Nchi 5 ambazo zimependekezwa na kupewa fursa ya kutekeleza mradi wa Global Biodiversity Framework.
Mradi wa Global Biodiversity Framework unalenga kuzuia upotevu wa bio-anuai kupitia mbinu za uhifadhi zinazoongozwa na jamii.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.