Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka Wazazi na Walezi mkoani umo kuwa sehemu ya uendelezaji wa vipaji vya watoto wao ili kuwawezesha kufikia ndoto zao.
Akizungumza kwenye Hafla ya ufunguzi wa mashindano ya michezo na Taaluma kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) kwa mwaka 2023 katika viwanja vya michezo Chuo cha ualimu Matogoro mjini Songea.
Kanali Thomas amesema Serikali imetenga Shule tatu za michezo mkoani wa Ruvuma lengo kuwakuza vijana kwenye Nyanja ya kitaaluma, michezo pamoja na kuwatafutia fursa za ajira.
“Yoyote kati yenu atakayeshindwa kutimiza wajibu wake katika maandalizi ya michezo maana yake awatakii mema watoto wetu mimi kama Mkuu wenu wa Mkoa nitafurahi kuona Ruvuma inakuwa namba moja kama ilivyo kuwa kwenye uzalishaji wa chakula katika sekta ya kilimo na sioni sababu kwanini na sisi tusiongoze katika michezo”
Mashindano hayo yana jumuisha wanafunzi 713 kutoka Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma pamoja na waalimu 60 ambao kwa pamoja wataunda timu ya Mkoa ili kwenda mkoani Tabora kushindana kitaifa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.