Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ametumia zaidi ya saa tatu kukagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo serikali imetoa shilingi bilioni 1.8 kutekeleza mradi huo unaojengwa eneo la Sanangula Kata ya shule ya Tanga.
Wananchi wa kata hiyo wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo ambao unakwenda kumaliza changamoto ya wananchi hao kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma ya afya.
Oktoba 26 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amekagua miradi mbalimbali katika Manispaa ya Songea inayogharimu shilingi bilioni 3.47.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Msingi Chief Zulu Academy inayojengwa kata ya Mshangano kwa gharama ya shilingi milioni 500,hospitali ya Manispaa ya Songea inayogharimu shilingi bilioni 1.8 na vyumba vya madarasa na mabweni sekondari ya Emanuel Nchimbi vinavyogharimu shilingi milioni 905.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.