MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka wananchi mkoani umo kuacha kusafisha mashamba kwa moto kwani uchomaji huo umeleta athari kubwa za kimazingira.
Kanali Thomas ameyasema hayo katika kijiji cha Liparamba wilayani Nyasa wakati alipofanya ziara na kuzungumza na wananchi alisema utaratibu wa kusafisha mashamba kwa kuchoma moto umepitwa na wakati hivyo amewataka viongozi wavijiji kuunda kamati za utunzaji mazingira
“Utunzaji wa mazingira ni jukumu letu sote, sisi wenyewe ni mashahidi miaka ya nyuma kipindi kama hiki mvua ingekuwa tayari imeshanyesha hii yote ni athari ambayo tunasababisha katika mazingira kwahiyo tuache kuchoma moto mashamba”amesema kanali thomas.
Mkuu wa Mkoa amesisitiza kwamba hakuna mtu yoyote anaye ruhusiwa kufanya shughuli zozote kwenye vyanzo vya maji hatahivyo ametoa maagizo kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kugawa miti kwa kila mwananchi kijiji hapo ifikapo Disemba, 1
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.