Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka Wakurugenzi na Viongozi wa Idara mbalimbali mkoani umo kupanda miti kwenye ofisi zao kwani uleta mandhari nzuri na utunzaji wa mazingira
Kanali Thomas ameyasema hayo leo januari 11,2023 wakati aliposhiriki uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti 1000 iliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) katika Shule ya Sekondari ya Limbo iliyopo Wilaya ya Nyasa
“Kila mtumishi leo hapa tukitoka kupanda miti apewe mti wake wa kwenda nao kupanda nyumbani itakuwa bora na kumbukumbu na watumishi wezangu kwenye ofisi zeto za Serikali tupande miti na tukipanda miti tutapata kivuli na kupenzesheza ofisi zetu”amesema Kanali Thomas.
Hata hivyo amewahimiza wanafunzi kuwa wasihishie kuipanda miti hiyo bali waitunze na kuiangalia kwani itawasaidia kuwapa kivuli muda wa mapunziko na kuhifadhi mazingira pia kuifanya Wilaya hiyo na Mkoa mzima wa Ruvuma kuwa wakijani
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.