Na Albano Midelo
Utafiti umebaini kuwa robo tatu ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ni hifadhi ikiwemo eneo la Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na ushoroba unayounganisha Selous na Niassa unaoanzia mkoani Ruvuma hadi nchini Msumbiji.
Kuna hifadhi tatu za jamii ndani ya Wilaya ya Namtumbo ambazo ni Mbarang’andu, Kisungule na Kimbanda.
Wilaya ya Namtumbo inahusika katika mradi mkubwa wa umeme wa bwawa la Nyerere katika Mto Rufiji unaoendelea kutekelezwa na serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mto Luegu unaonzia Wilaya ya Namtumbo unachangia asilimia 19 ya maji katika Mto Rufiji hivyo Mkoa wa Ruvuma unahusika moja kwa moja na uendelevu wa mradi wa bwawa la Nyerere katika Mto Rufiji ambao umekusudia kuondoa mgawo wa umeme nchini.
Utalii wa uwindaji unaofanyika katika Jumuiya ya Hifadhi ya wanyamapori ya Mbarang'andu wilayani Namtumbo imekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka nchi za Ulaya na Marekani ambao wanatembelea jumuiya hiyo yenye vijiji saba na kufanya aina hiyo ya utalii ambayo inahusisha moja kwa moja matumizi ya wanyamapori.
Jumuiya hiyo inahusisha vijiji saba ambavyo ni Mchomolo, Kitanda, Likuyuseka Maganga, Kilmasela, Nambecha, Songambele na Mtelemwahi.
Afrikanus Challe ni Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma anasema utalii wa uwindaji unafanyika katika mapori ya akiba yaliyopo sehemu mbalimbali nchini na kwamba aina hiyo ya utalii inakwenda sanjari na utalii wa picha ambao ni utalii wa kutazama mandhari na kupiga picha bila kuhusisha uwindaji wa wanyama na kwamba utalii wa picha pia husisha matumizi ya moja kwa moja ya wanyamapori.
Mradi wa bwawa la Mwl. Nyerere katika Mto Rufiji ambao umekusidia kumaliza tatiizo la mgawo wa umeme nchini
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.