MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema wameshiriki katika zoezi la kufanya Usafi Soko la Bombambili.
Zoezi hilo la usafi limefanyika kwa kuwakumbuka Mashujaa Tanzania waliopigania Uhuru wa Nchi ya Tanzania ametoa wito kwa wananchi kuwa zoezi la usafi liwe endelevu.
Ameseama kila mwaka Julai 25 tunaadhimisha kumbukizi ya mashujaa kwa shughuli mbalimbali ikiwemo usafi.
Hata hivyo amesema usafi ni sehemu ya utunzaji wa mazingira
“Sisi sote tunajua umuhimu wa mazingira kama sehemu ya uzalendo tuhakikishe tunatunza mazingira kwa namna mbalimbali kama vile kupanda miti ya aina mbalimbali kwasababu miti ni uhai”.
Ametoa wito kwa wakazi wa Songea kuhusu kutunza mazingara kama kumbukizi ya mashujaa.
Mgema ametoa rai kwa wananchi kujitokeza katika zoezi la sensa ifikapo Agosti 23 amesema ili nchi iweze kujipanga kiuchumi na kibajeti lazima ijue idadi ya watu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dr.Fredirick Sagamiko amewapongeza wananchi kwa kujitokeza katika zoezi la usafi na amewaahidi ifikapo Julai 29,2022 Soko hilo litakuwa limeezekwa na wafanyabiashara watafanya kazi zao katika mazingira mazuri.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.