• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RUVUMA yaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kwa kishindo,serikali,jamii na wazazi waungana kumlinda mtoto

Imewekwa kuanzia tarehe: June 16th, 2025

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kimkoa yaliyofanyika Juni 16, 2025, katika Halmashauri ya Madaba, wilayani Songea, yamesisitiza umuhimu wa jamii, Serikali, wazazi na wadau wote kuungana kuwalinda, kuwatunza na kuwaendeleza watoto, kama hazina ya taifa la kesho.

Hafla hiyo, iliyohudhuriwa na mamia ya wananchi, iliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mheshimiwa Ngollo Malenya, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed.

 Katika hotuba yake, Malenya aliwakumbusha Watanzania historia ya Siku ya Mtoto wa Afrika, inayotokana na maandamano ya watoto wa Soweto, Afrika Kusini, Juni 16, 1976, maandamano yaliyokuwa yakipinga mfumo wa elimu wa kibaguzi na hatimaye kusababisha vifo, kujeruhiwa, na mateso ya mamia ya watoto.

“Siku ya Mtoto wa Afrika ni fursa ya pekee ya kutafakari; tulipotoka, tulipo, na tunapoelekea. Kauli mbiu ya mwaka 2025,Haki za Mtoto: Tulipotoka, Tulipo na Tuendako inatukumbusha sote kuwa mustakabali wa watoto upo mikononi mwetu. Tukiwekeza kwa watoto, tunawekeza kwa taifa zima.” Alisisitiza Malenya.

Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya 2022 zinaonesha mkoa wa Ruvuma una watoto 855,106, wakiwakilisha asilimia 46.3 ya idadi ya watu 1,848,794. Kati ya watoto hao, wavulana ni 428,058 na wasichana 427,048.

 Takwimu hizo zinabainisha dhahiri wajibu wa jamii na Serikali kutoa kipaumbele kwa malezi, ulinzi, elimu, na afya ya watoto.

Serikali, kupitia Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya 2008, Sheria ya Mtoto Na. 21 ya 2009 (pamoja na marejeo ya 2019), madawati ya ulinzi wa watoto, na Programu ya Shule Salama, imetenga rasilimali na mifumo ya kisheria inayolenga kuhakikisha watoto wanapata haki ya kuishi, kupendwa, kulindwa, kutobaguliwa, kuendelezwa, na kushirikishwa.

Akihutubia umati wa wananchi, Malenya alisisitiza: “Serikali ya Tanzania inatekeleza sera hizi kwa vitendo. Majengo ya madarasa, madawati ya ulinzi, dawati la jinsia na watoto, huduma za afya, na ruzuku ya elimu ni mifano hai ya jinsi Serikali inavyothamini maisha ya watoto.”

Hata hivyo, Malenya alibainisha changamoto zinazoukabili mkoa, kama vile baadhi ya wazazi kutowajibika, watoto kuishi mitaani, na kuongezeka kwa visa vya ukatili.

Alitolea mfano wa takwimu za Polisi mkoani Ruvuma, zinazonesha kwamba takriban visa 30 hadi 40 vya ukatili wa kingono huripotiwa kila mwaka, lakini vingi havifikishwi mahakamani kutokana na ushirikiano mdogo wa familia.

“Tunawasihi wazazi, walezi na jamii nzima, tusifumbie macho vitendo vyovyote dhidi ya watoto. Tushirikiane na vyombo vyetu, kama madawati ya jinsia, polisi, na ustawi wa jamii, kutoa ushahidi na kuhakikisha haki inatendeka.” Alisisitiza Malenya.

Akisoma risala ya watoto, mmoja wa wawakilishi wa watoto wa Madaba alisema: “Tunashukuru Serikali kwa madawati ya ulinzi, ruzuku ya elimu, na uboreshaji wa huduma. Lakini tunaomba jamii itimize wajibu wake wa malezi. Watoto wengine wanaishi mitaani, wanabaguliwa, wanaonewa, na kunyanyaswa. Tunaomba jamii itulinde, itupende, na ituheshimu.”

Hotuba hiyo ya watoto ilibainisha pia mafanikio yaliyopatikana, kama ujenzi wa madarasa, kuongezeka kwa madawati, na uwepo wa dawati la ulinzi wa watoto shuleni, lakini ikasisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano wa jamii.

Siku ya Mtoto wa Afrika inatufundisha kwamba watoto ni urithi wa kesho. Wakiandaliwa vyema, wataleta maendeleo, amani, na ustawi wa taifa. Hii ni fursa ya pekee kwa Serikali, jamii, wazazi na wadau wote kuungana, kupanga, na kutekeleza mikakati ya kuwalinda, kuwaendeleza na kuwatunza watoto

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RUVUMA yaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kwa kishindo,serikali,jamii na wazazi waungana kumlinda mtoto

    June 16, 2025
  • WAKULIMA Ruvuma waomba soko la mahindi kufunguliwa haraka

    June 16, 2025
  • SERIKALI ,dini na wananchi Ruvuma waungana kudumisha amani

    June 16, 2025
  • RUVUMA yaandika historia chupa 4040 za damu zakusanywa kuokoa maisha

    June 15, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.