Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki imekagua eneo la ujenzi wa shule mpya ya msingi Suluti Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ambapo serikali kupitia mradi wa BOOST imetoa shilingi milioni 331.6 kutekeleza mradi huo.
Majengo yanayojengwa ni madarasa saba,jengo la Utawala,madarasa mawili ya awali,matundu kumi ya vyoo,kichomea taka na ujenzi wa wigo.
Sekretarieti ya Mkoa imetembelea eneo la mradi ambao unatarajia kuanza kutekelezwa wakati wowote katika eneo lenye ukubwa wa hekari 15.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.