Serikali imetenga zaidi ya Shilingi bilioni nne kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji safi na salama kwa wakazi zaidi ya 60,868 wa kata nane katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga, mkoani Ruvuma.
Mradi huu unajumuisha ujenzi wa vyanzo viwili vya maji vyenye uwezo wa kuzalisha lita 1,613,200 kwa siku, matenki manne yenye ujazo wa lita 525,000, pamoja na mtandao wa mabomba wa kilomita 57.
Lengo ni kuhakikisha huduma ya maji inafikia asilimia 97.8 katika maeneo yanayonufaika na mradi huu.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbinga (MBIUWASA ), Mhandisi Yonas Ndomba, alisema kuwa mradi huu utapunguza uhaba wa maji uliopo.
Ameyataja Kwa sasa, mahitaji ya maji mjini Mbinga ni lita 5,478,000 kwa siku, lakini uzalishaji upo kwenye lita 3,797,000 pekee.
Utekelezaji wa mradi huu utafanywa na Kampuni ya Ngogo Engineering Ltd kwa gharama ya Shilingi milioni 755,194,120.25, huku Kampuni ya Simba Pipe Industries Ltd ikihusika na utengenezaji na usambazaji wa mabomba kwa gharama ya Shilingi bilioni 3,255,414,297.38.
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mheshimiwa Kisare Makori, amezitaka kampuni husika kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa viwango bora.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya MBIUWASA, Mhandisi Patrick Ndunguru, amewataka watendaji wa mamlaka hiyo kumsimamia mkandarasi kwa karibu ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati ili wananchi wanapata maji bila kuchelewa.
Kupitia mradi huu, Halmashauri ya Mbinga Mji inatarajiwa kufikia asilimia 98.3 ya upatikanaji wa maji safi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.